Mwanamke kumuwekea sharti mume wasizae

Swali: Mke akimuwekea sharti mume wake wakati anapomuoa wasizae. Ni ipi hukumu ya sharti hii?

Jibu: Sharti hii sio sahihi. Sharti batili. Kwa kuwa kuzaa kunatakikana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Oeni wanawake wenye kizazi. Hakika mimi nitajifakhari kwa wingi wetu na Ummah zingine siku ya Qiyaamah.”

Kuzaa ni jambo linalotakikana. Mwenye kuwekea sharti ya kutozaa, sharti hii sio sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/files/ls–jeddah-1430-8-17.mp3
  • Imechapishwa: 25/09/2020