Swali: Ni ipi hukumu mwanaume akamfanyia Hajj mwanamke au kinyume chake na inatosheleza?

Jibu: Ndio, inajuzu kwa mwanamke kumfanyia Hajj mwanaume. Kwa kuwa kuna mwanamke alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba baba yake faradhi ya Hajj imemkuta akiwa Hajj na yeye hawezi kupanda vizuri juu ya mpando, kutokana na utuuzima, akamwambia “Muhijie baba yako”. Mwanamke anaweza kumhijia mwanaume na mwanaume akamhijia mwanamke. Hakuna kizuizi kwa hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1431-04-12.mp3
  • Imechapishwa: 14/11/2014