Mwanamke kukata swawm ya deni la Ramadhaan kwa ajili ya kustarehe na mume wake

Swali: Kuna mwanamke amelipa Swawm ya Ramadhaan. Je, inajuzu kwake kula katikati ya mchana ili aweze kukaa na mke wake?

Jibu: Hapana. Kila Swawm ambayo ni ya wajibu kukiwemo ya kafara, mtu akishaiingia ndani yake, ni wajibu kukamilisha siku. Anayeingia katika (Swawm ya) faradhi ni haramu kuikata. Akamilishe siku. Ama kuhusu Naafilah, hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (65) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13832
  • Imechapishwa: 16/11/2014