Mwanamke kujitia manukato anapotoka nje ya nyumba

Swali: Je, inafaa kwa mwanamke anapotaka kwenda masomoni, hospitali au kuwatembelea ndugu na jamaa akajitia manukato?

Jibu: Inafaa kwake kujitia manukato ikiwa kutoka kwake ni kwenda kwenye mkusanyiko wa wanawake na njiani hatopita karibu na wanamme. Lakini kujitia kwake manukato hakutojuzu ikiwa atatoka kwenye masoko ambayo wako wanamme. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanamke yeyote atayepatwa na uvumba, basi asishuhudie pamoja nasi ´Ishaa.”

Zipo Hadiyth nyingine zilizopokelewa juu ya jambo hilo.

Isitoshe kutoka kwake nje akiwa na manukato katika njia za wanamme na mkusanyiko wa wanamme – kama mfano wa misikiti – ni miongoni mwa sababu zinazopelekea katika fitina. Kadhalika ni lazima kwake kujisitiri na kuhadhari kuonyesha mapambo. Amesema (´Azza wa Jall):

وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاهِلِيَّةِ الْأُولَى

“Tulizaneni majumbani mwenu na wala msijishauwe kwa kuonyesha mapambo kama walivyojishauwa zama za ujahili.”[1]

Miongoni mwa kuonyesha mapambo ni kuonyesha yale mapambo na uzuri ikiwa ni pamoja na kuonyesha uso, kichwa na vyenginevyo.

[1] 33:33

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/40)
  • Imechapishwa: 05/08/2021