Mwanamke kufungishwa ndoa na baba kafiri


Swali: Muislamu akitaka kuoa mwanamke wa Kiislamu inawezekana baba yake kafiri akawa ndio walii wake katika ndoa?

Jibu: Hapana. Kafiri hana utawala wowote juu ya Muislamu mwanamke. Hili litasimamia Waislamu. Mtawala ndio atamfungisha ndoa au mahakama ya Kishari´ah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (53) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-06-12.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014