Swali 205: Umesema kwamba hakuna ubaya mwanamke kuendesha gari. Unaonaje iwapo mwanamke atasafiri na gari kutoka Swa´idah kwenda Swa´aa’? Je, kitendo hichi si ni khatari kwake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke anayemwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Ikiwa mwanamke ndiye anayejua kuendesha na mume wake au mtoto wake wa kiume ambaye tayari ana uwezo wa kupambanua mambo hajui hakuna neno akaendesha. Sijui kikwazo juu ya jambo hilo. Kinachozingatiwa ni dalili. Mwenye kudai kwamba haijuzu basi ni juu yake kuleta hoja. Nimeshatangulia kusema kwamba kitendo hichi sikipendelei na wala sikiridhii kwa mke wangu. Lakini masuala ya uharamu au uhalali yanahitajia dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 408
  • Imechapishwa: 06/10/2019