Swali: Tunaomba nasaha kwa wanawake kwa kuchonga meno, kurefusha nywele na kuvaa suruwali.

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamlaani mchonga meno na mwenye kuchongwa. Wote wamelaaniwa anayefanya na kufanyiwa na wanashirikiana katika laana.

Suruwali si katika mavazi [ya mwanamke]. Si katika mavazi ya wanaume kwetu, vipi yatakuwa katika mavazi ya wanawake? Kutokana na fitina ilionayo, kwa kuwa inadhihirisha mwili wa mwanamke viungo visivotakiwa kuonekana vya mwanamke. Sio katika mavazi ya waislamu wanawake katika nchi hii [Saudi Arabia]. Mwanamke avae mavazi ya wanawake wa Kiislamu katika nchi hii. Hili ndilo linalohitajika.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://youtu.be/hDWCQFz3Bhs
  • Imechapishwa: 07/09/2020