Mwanamke kama huyu ni haramu kwake harufu ya Pepo

Swali: Imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Mwanamke yeyote ambaye atamuomba mume wake talaka pasi na kosa basi ni haramu juu yake harufu ya Pepo.”

Je, mwanaume akioa juu yake mwanamke wa pili ni miongoni mwa sababu au kosa la kumfanya yeye kuomba talaka kwa sababu hii?

Jibu: Hapana. Akitaka aoe wanawake watatu juu yake. Hii ni haki yake. Asipingane nae. Lakini hata hivyo afanye uadilifu. Hii ni sharti. Afanye uadilifu kati yao. Asimdhulumu mmoja wao au akapinda kwa mmoja wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 03/11/2017