Mwanamke kafariki na deni afungiwe na jamaa zake?

Swali: Kuna mwanamke aliekufa naye alikuwa na deni la Ramadhaan. Je ni wajibu kwa jamaa zake kama watoto wake kumfungia au kulisha?

Jibu: Ndio, wamfungie. Kama alivyosema Mtume (swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atayekufa naye anadaiwa swawm, basi amfungie walii wake.”

Wamfungie. Isipokuwa ikiwa alishikwa na maradhi mpaka akafa hivyo akawa hakuweza kufunga, watakuwa hawana ulazima wowote wa kulipa. Ama ikiwa aliweza kulipa na hakufanya hivyo, au kula kwake haikuwa kwa sababu ya maradhi, bali ilikuwa ni kwa sababu ya nifasi au hedhi. Huyu atalipiwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://alwasabi.al3ilm.com/alfatawaa
  • Imechapishwa: 10/05/2020