Mwanamke huyu ni kama aliye msafi


Swali: Ni ipi hukumu mwanamke akitumia dawa inayokata nifasi au hedhi katika masiku yake?

Jibu: Mwanamke akitumia vidonge au sindano ambapo damu yake ikakatika, basi anatakiwa kuoga na kufanya yale yanayofanywa na wanawake waliowasafi. Hapo swalah na swawm zake vitakuwa ni sahihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (15/200)
  • Imechapishwa: 24/05/2018