Mwanamke hawi Mahram wa mwanamke mwenzie


Swali: Je, mwanamke anahesabiwa kuwa ni Mahram kwa mwanamke mwenzie wa kando safarini?

Jibu: Mwanamke sio Mahram kwa mwenzie. Mahram ni mwanamme ambaye ameharamika kwa mwanamke huyo kutokana na nasaba. Kwa mfano baba au kaka yake. Mahram pia anaweza kuwa anatokana na sababu iliyoruhusiwa kama mfano wa mume, baba yake mume, mtoto wake mume, babako anayetokana na mkewe kukunyonyesha, kaka yako ambaye mlinyonya ziwa moja na mfano wa hao.

Haijuzu kwa mwanamme kukaa chemba na mwanamke wa kando. Wala pia haifai kusafiri naye. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Asisafiri mwanamke isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamme hakai faragha na mwanamke isipokuwa watatu wao huwa ni shaytwaan.”

Ameipokea Ahmad na wengineo kupitia kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (08/336)
  • Imechapishwa: 18/06/2021