Mwanamke aswali swalah ya kupatwa kwa jua nyumbani au msikitini?

Swali: Ni bora kwa wanawake kuswali nyumbani [swalah ya kupatwa kwa jua] au pamoja na mkusanyiko wa waislamu?

Jibu: Bora ni mwanamke kuswali nyumbani kwake. Isipokuwa swalah moja tu; nayo ni swalah ya ´Iyd mbili. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha wanawake watoke, lakini hata hivyo watoke hali ya kuwa si wenye kuonyesha mapambo na wala wenye kujitia manukato. Ama kuhusiana na swalah zengine hakuna neno kwa mwanamke kuswali pamoja na wanaume msikitini na khaswakhaswa swalah ya kupatwa kwa jua.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1114
  • Imechapishwa: 17/04/2019