Mwanamke anayeishi pembezoni mwa msikiti kumfuata imamu


Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye anaishi jirani ya Msikiti na kati kuna ukuta unaoweka mpaka kumfuata Imamu Ramadhaan katika Tarawiyh na akaswali naye?

Jibu: Hapana. Ikiwa mahala ambapo yuko ni sehemu katika Msikiti, hakuna neno. Ama ikiwa sio katika Msikiti, asimfuati Imamu isipokuwa ikiwa kama anamuona Imamu au anamuona mtu alie nyuma yake. Ama kusikia tu sauti ilihali hayuko Msikitini, haijuzu kumfuata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (55) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo--1432-10-13.mp3
  • Imechapishwa: 16/11/2014