Mwanamke anaweza kuonyesha mikono na miguu katika swalah?   

Swali: Ni lazima kwa mwanamke asujudie juu ya tumbo la viganja vyake pasi na kuwa na kizuizi na vilevile miguu yake miwili?

Jibu: Hapati kufanya hivo. Mwanamke anatakiwa kusujudu juu ya ardhi ilihali amesitiri viganja vyake na miguu yake. Wanachuoni wengi wanaonelea kuwa viganja na miguu ya mwanamke ni ´Awrah katika swalah ambavyo ni lazima kwa mwanamke avifiche. Ilikuwa ni katika ada ya mwanamke wa Maswahabah kuvaa vifuniko vya mikono kwa sababu vinamsitiri. Haina neno endapo hatoigusa ardhi moja kwa moja.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (05)
  • Imechapishwa: 02/05/2020