Mwanamke anaweza kufungishwa ndoa na kaka yake wa kuchangia ziwa?

Swali: Je, inajuzu kwa kaka wa kuchangia ziwa akamuozesha dada yake wa kuchangia ziwa ikiwa mwanamke huyu hana walii wa kumuozesha au kuozeshwa kwake kunakuwa kwa Qaadhiy?

Jibu: Wale wote ambao ana mafungamano nao kwa kuchangia ziwa moja hawana haki ya kumuozesha. Baba yake kwa sababu ya unyonyeshaji haifai akamuozesha. Kaka yake kwa sababu ya unyonyeshaji haifai akamuozesha. Kwa sababu hakuna nasabu kati yao wao na mwanamke huyo. Tunasema kwamba mwanamke hafungishwi ndoa isipokuwa tu na wale ndugu zake wavulana kinasabu. Hii ndio kanuni yenyewe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (55) http://binothaimeen.net/content/1259
  • Imechapishwa: 02/10/2019