Mwanamke anatoa darsa msikitini na hakusoma kwa wanachuoni

Swali: Mwanamke ambaye ni mtafutaji elimu kwa njia ya vitabu na mikanda iliyotarjumiwa. Na yuko na uwezo wa kuwasiliana na wanachuoni wakati mambo yanapomtatiza. Je, anaweza kuwafunza wanawake wenzake Msikitini kutokana na kukosekana kuwa mwanamke mwingine awezae kuwafunza kuhusu mambo ya ´Aqiydah na Manhaj.

Jibu: Ni jambo linalojulikana ya kwamba mtu anatakiwa kuchukua elimu moja kwa moja kutoka kwa wanachuoni. Na achukue kila fani ya elimu kwa mtu ambaye kabobe katika fani ya elimu hiyo. Wakati anapotaka kuchukua elimu ya Tafsiyr ya Qur-aan, aichukue kwa mtu ambaye kabobea katika elimu hii. Hali iwe namna hii katika elimu zingine. Hii ni njia ya kwanza.Njia ya pili ni ya mtu kusoma vitabu. Lakini asisome vitabu na kuvitegemea isipokuwa ikiwa ni mwenye upeo wa kuvifahamu kwa njia sahihi. Kwa kuwa ikiwa yuko na mapungufu katika ufahamu wake, huenda akafahamu kitu kinyume na usawa wake. Matukio yake ikawa akaenda kuongea kwa alivyofahamu na yale atakayoongea yakawa ni ya makosa. Akawafunza watu yale aliyofahamu kwa njia ya makosa. Akaja kubeba madhambi yao. Kwa nisba ya mwanamke huyu, mimi namnasihi asifunze kutokana na kwamba anasoma vitabu bila ya kuwa na mtu wa kumfahamisha navyo vitabu hivi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdillaah al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.sahab.net/forums/index.php?app=forums&module=forums&controller=topic&id=134918
  • Imechapishwa: 16/03/2018