Mwanamke anatakiwa kuyatolea zakaah mapambo yake ya dhahabu na fedha

Swali: Dhahabu anayotumia mwanamke anatakiwa kuitolea zakaah hata kama hana pesa ya kuitolea zakaah wala haweki akiba katika mshahara wake wa kila mwezi?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba anatakiwa kuitolea zakaah pale inapofikisha kile kiwango cha lazima. Wanazuoni wamekhitilafiana. Maoni sahihi ni kwamba inatolewa zakaah. Dhahabu na fedha – ni mamoja vinatumiwa au havitumiwi – vinatakiwa kutolewa zakaah kwa ambaye anavimiliki katika wanamme au wanawake pale vinapofikisha kile kiwango cha lazima. Kiwango cha lazima ni mithqaal 20 ambapo ni 92 g. Dhahabu inapofikisha kiwango hicho basi ni lazima kuitolea zakaah. Haijalishi kitu anaitumia au haitumii. Hukumu ni moja.

Kuhusu almasi na mawe mengine ya thamani ambayo yanatumiwa hayatolewi zakaah. Isipokuwa ikiwa yameandaliwa kwa ajili ya biashara.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4420/حكم-ومقدار-زكاة-الحلي-المعد-للزينة
  • Imechapishwa: 17/06/2022