Swali: Ipi hukumu ya mwanamke kufanya kazi ya udaktari, ualimu na zisizokuwa hizo?

Jibu: Haya ni mabalaa ambayo wamepewa majaribio kwayo Waislamu na kupotea kwa sababu yake. Mwanamke anatakikana kuolewa naye ni msichana wa miaka 13, 14 au 15. Namna hii ndivyo inavyotakikana. Lakini yeye anataka kukamilisha masomo yake; Thanawiy, chuo kikuu, masta, Dr. kisha baada ya hapo anatoka kama mwalimu na ikiwa ni mke wa mtu analeta mfanya kazi nyumbani. Anashindwa kumpa mtoto malezi na maadili ya Kiislamu. Muhimu ni kuwa, Waislamu hawahukumu kwa Shari´ah ya Allaah katika jambo hili.

Na wajibu kwetu sote tuhukumu kwa Shari´ah ya Allaah. Mwanamke bora kwake ni yeye kuwa nyumbani kwake. Na kutoka kwake, huzingatiwa ni fitina kwake yeye au kwa wengine. Haitakikani kwa yeyote kutoa idhini ya kufunza, isipokuwa tu ikiwa kama ni kufunzana Qur-aan na anajiwa na watu nyumbani kwake au anatoka na wala hachanganyiki na wanaume. Ama kufunza au kusoma katika masomo tulionayo na mchanganyiko kwenye chuo kikuu, hili ni jambo lisilojuzu kwa hali yoyote ile, kwani huzingatiwa kuwa ni fitina.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1111
  • Imechapishwa: 28/02/2018