Mwanamke anatakiwa kujiheshimu kwa mavazi yake


Swali: Ni upi mpaka wa ´awrah ya mwanamke mbele ya mwanamke mwenzie?

Jibu: Ni kuanzia kwenye kitovu mpaka kwenye magoti. Mwanamke anatakiwa kujiheshimisha. Hatakiwi kuacha wazi mgongo, mikono na muundi wake. Kwa sababu kufanya hivo ni uchache wa haya. Asithubutu kufanya kitendo hicho. Anaweza kuwa mahali ambapo wanafika wanamme kama mfano wa harusini. Pengine baadhi yao wanaingia ndani. Kufanya hivo inaweza kuwa ni sababu ya kuonyesha sehemu ya uchi wake anapokuwa barabarani au ndani ya gari. Kwa hivyo ni lazima kwa mwanamke kujiheshimu ingawa atakuwa kati ya wanawake peke yao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (19)
  • Imechapishwa: 26/02/2021