Swali: Kuna mwanamke ambaye anasikiliza darsa zenu kwa mara ya pili. Anasikia kunasemwa kuhusu Madaakhilah na kwamba wana msimamo mkali katika dini. Anatafuta haki na anaomba nasaha, maelekezo na kumuombea du´aa juu ya mafanikio yake.

Jibu: Aendelee kusikiliza na kufuatilia darsa. Atastafidi kwa uwezo na nguvu za Allaah. Atasikia haki, ´Aqiydah sahihi, hukumu za Kishari´ah, utahadharisho wa yaliyokatazwa na mielekeo mizuri kuhusiana na kujua haki za Allaah juu ya waja na haki za watu baina yao.

Asiwasikilize wale wanaosema kuwa Madaakhilah wana msimamo mkali. Kilichopo kwao ni kubainisha haki, kulingania watu katika hiyo haki na kuifanyia kazi. Wewe endelea kusubiri na kufuatilia darsa.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://z-salafi.com/v2/action?s_menu=23&idFatwa=2399
  • Imechapishwa: 26/06/2020