Swali: Baadhi ya ndugu wanataka kuoa mke wa pili, anamuomba udhuru na huku anasema ya kwamba Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah Hakalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya uwezo wake.” (02:286)

Na yeye hawezi kuvumilia kuolelewa juu yake mwanamke mwengine. Anasema kama unataka kuoa mke mwengine, nitaliki.

Jibu: Aula kwake ni yeye asubiri mpaka pale atapoona sio muadilifu, hapo kutakuwa hakuna neno akaomba waachane. Na Allaah (´Azza wa Jalla) Anasema:

فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ

“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake; wawili au watatu au wanne.” (04:03)

Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mwenye kuoa wanawake, isipokuwa tu haijuzu kuoa wanawake zaidi ya wanne. Kinachohitajika ni yeye kuwa muadilifu. Ikiwa ni mwanamke mwema na anataka kusubiri naye, hili ni jambo halina ubaya. Na ikiwa si mwanamke mwema, hakuna ubaya akatengana naye na akaoa mwanamke mwema. Tanabahi! Haijuzu kwake (mwanamke) kuitakidi kuwa ni haramu kuoa mke mwengine. Ama ikiwa hawezi kuvumilia… Sisi tunamnasihi aweze kuvumilia mpaka hapo atapoona kuwa sio muadilifu, la sivyo lau ataamini kuwa jambo hili ni haramu, huchukuliwa ni kufuru. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anamwambia ´Aliy bin Abiy Twaalib alipokuwa anataka kuoa binti wa Abu Jahl, akamwambia: “Naapa, hawezi kukusanyika binti wa Mtume wa Allaah na binti wa Abu Jahl. Akitaka ´Aliy kuoa binti wa Abu Jahl, atengane na binti yake (Faatwimah).” Au maneno ya kufanana na hayo. Muhimu tu asiamini kuwa kufanya hivyo ni Haramu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2757
  • Imechapishwa: 29/12/2017