Mwanamke anasafiri kwa ndege dakika 90 bila ya Mahram

Swali:  Ni ipi hukumu ya mwanamke kusafiri peke yake bila ya Mahram ikiwa safari hiyo ya ndege inachukua saa moja na nusu?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke kusafiri umbali wa siku mbili bila ya kuwa na Mahram au mume wake.”

Bi maana na mnyama. Ni kiasi na kimomita 80. Si halali kwake kusafiri isipokuwa awe na Mahram sawa ikiwa ni kwa ndege, gari, mnyama au kwa kutembea. Ni lazima awe na Mahram. Hili ni hata katika hajj; asihiji isipokuwa awe na Mahram. Kuna mwanaume alisema: “Ee Mtume wa Allaah! Mke wangu ameenda kuhiji na mimi nimeandikwa kwenda na kikosi vitani”. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:

“Rejea na uhiji na mke wako.”

Amerudishwa na kikosi cha vita ili aweze kwenda kuhiji na mke wake. Hivi sasa wapo wenye kusema kuwa mwanamke anaweza kusafiri na ndege bila ya Mahram. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amezungumza kwa kuenea na hakuvua kitu. Linatumika katika kila zama, sehemu na katika hali zote. Yule anayemcha na kumwogopa Allaah ni lazima asafiri na Mahram. Ama kuhusu yule anayetaka kufanya ujanja na kutafuta watu wanaoweza kumpa fatwa, huyu hesabu yake iko kwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (19) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf%2030-7-1434_01.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2020