Swali: Baadhi ya wanawake wanasoma katika chuo kikuu cha mchanganyiko. Wanapoambiwa wasifanye hivyo, wanasema kuwa wanajitengenezea Mustaqbal wao. Isitoshe, mwanamke huyu anasafiri bila ya Mahram. Ni ipi hukumu ya Kishari´ah kwa hilo?

Jibu: Mwanamke anayesoma katika chuo kikuu ambacho ni mchanganyiko, huzingatiwa kuwa ni mwenye kukosea na anapata madhambi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema, katika Hadiyth ambayo imepotea Usaamah bin Zayd (Radhiya Allaahu ´anhu):

“Sijaacha fitina iliokuwa kubwa kwa wanaume kama wanawake.” Na anasema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wanawake ni wenye akili na Dini pungufu.”

Mwanaume anaenda na kutaka kumchumbia kwa familia yake, hapo kafikisha miaka 25. Anaambiwa karibu, ila haitowezekana isipokuwa mpaka baada ya kumaliza masomo yake. Lini atamaliza masomo yake chuo kikuu? Baada ya miaka 52. Anamaliza masomo huku kishakuwa mzee na havutii tena. Ilihali lau angeliolewa katika usichana wake, angelikuwa amekwishazaa watoto watano, sita, saba n.k., kwa kiasi ambacho Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) Atakuwa Amempa. Tunamnasihi kuacha masomo haya. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Yule mwenye kuacha kitu kwa ajili ya Allaah, Allaah Humpa kilicho bora kuliko hicho alichoacha.”

Muulizaji: Kusafiri bila ya kuwa pamoja na Mahram?

al-Waadi´iy: “Sio Halali kwa mwanamke ambaye anamwamini Allaah na siku ya Mwisho kusafiri bila ya kuwa pamoja naye Mahram.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2303
  • Imechapishwa: 24/02/2018