Swali: Je, ndoa inaathirika ikiwa mwanamke atanuia Tahliyl[1] kwa ndoa hiyo?

Jibu: Ndio. Ndoa inabatilika ikiwa atanuia hivo. Ikiwa mmoja wa wanandoa atanuia hivo, hilo linabatilisha ndoa hiyo.

[1] [1] Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:

”Ndoa nyingine iliyoharamishwa na Allaah (´Azza wa Jall) na imetokea kwa baadhi ya watu ni ndoa inayoitwa “kufanya halali”, Tahliyl. Pindi mwanamume anapomtaliki mke wake kwa mara ya tatu na hivyo anakuwa hawezi kumrudi tena, anakubaliana na mwanaume mwingine ili amuoe. Pindi yule mume wa pili anapomuoa na kumwingilia, anamtaliki ili aweze kurudi kwa yule mume wake wa kwanza. Hii ndio ile ndoa inayoitwa “Tahliyl” na inafanywa na watu wenye imani dhaifu na wasiomcha Allaah (´Azza wa Jall). Imethibiti kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Allaah amlaani yule mwanaume anayefanya halali na yule mwanaume anayehalalishiwa.” (Ibn Maajah (1963). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (1585)) http://www.alifta.net/Fatawa/FatawaChapters.aspx?languagename=ar&View=Page&PageID=3998&PageNo=1&BookID=4

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (59) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-29-01-1438_0.mp3
  • Imechapishwa: 27/10/2017