Mwanamke anamkasirisha mume wake wa pili ili arudi kwa yule wa kwanza


Swali: Kuna mwanaume ameachana na mke wake talaka ya tatu kisha akataka kumrejea. Akaolewa na mwanaume mwengine kisha akaanza kumfanyia vitimbi ili kumkasirisha kwa lengo amtaliki. Je, inafaa kwake kufanya hivo?

Jibu: Hapana. Ni haramu kwa mwanamke huyo kufanya hivo. Anafanya hivo ili aweze kurudi kwa yule mume wa kwanza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017