Mwanamke anakata nywele zake na anavaa suruwali kwa ajili ya mume


Swali: Ni ipi hukumu juu ya kukata nywele na kuvaa suruwali kwa ajili ya mume?

Jibu: Uzuri unapatikana katika nywele za mwanamke na sio katika kuzikata. Yeye kukata ina maana anajifananisha na wa magharibi na wanawake ambao hawajali uzuri wao. Nywele za mwanamke ndio mapambo yake na aziache kama zilivyo na asikate chochote katika hayo.

Ama kuhusiana na suruwali, hivyo haijuzu kwa mwanamke kuvaa suruwali. Inaonesha maumbile yake. Suruwali sio katika mavazi ya nchi hii. Inakwenda kinyume na haya na kujisitiri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/node/5405
  • Imechapishwa: 07/09/2020