Swali: Ipi hukumu ya mwanamke ambaye ametalikiwa kisha akaolewa na mwanaume mwingine. Na baada ya muda mrefu akamuomba yule mume wake wa kwanza kumwandikia Talaka ili kupata pesa kutoka serikali, pamoja na kuwa (mwanamke huyu) kwa sasa yuko katika dhimma ya mwanaume ambaye yuko nae sasa?

Jibu: Ni kama tulivyosema. Hata kama itakuwa ni kweli katalikiwa, lakini akaficha ukweli ya kwamba kaolewa (na mume mwingine) baada ya hapo, haya ni maovu na utatizi. Ndani yake kuna hila na uadui. A´udhubi Allaah. Kuchukua mali pasina haki ni jambo ovu na ni ulaji wa vya Haramu. Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Nuur ´alaad-Darb
  • Imechapishwa: 17/03/2018