Mwanamke ana vazi maalum katika Ihraam?

Swali: Je, mwanamke ana vazi maalum katika Ihraam? Ni ipi hukumu ya kubadilisha mavazi ya Ihraam sawa kwa mwanaume au mwanamke?

Jibu: Mwanamke hana vazi maalum katika Ihraam. Avae anachotaka. Isipokuwa asionyeshe mapambo. Ana ruhusa ya kubadilisha mavazi kwa sababu ya uchafu, najisi au mengineyo. Kadhalika mwanaume ana ruhusa ya kubadilisha mavazi ya Ihraam. Lakini inatambulika kuwa mwanaume ana mavazi maalum katika Ihraam; kikoi na Ridaa´ (shuka). Lakini endapo atataka kuyabadilisha hakuna neno ima kwa sababu ya uchafu, najisi au sababu  nyengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (73) http://binothaimeen.net/content/1708
  • Imechapishwa: 16/04/2020