Mwanamke ametubia baada ya miaka mingi kutoswali na kutofunga

Swali: Mimi ni muheshimiwa wa kike ambaye nina watoto. Miaka mitatu iliyopita sikuwa ni mwenye kuswali wala kufunga. Lakini hivi sasa Allaah ameniongoza naswali, nafunga, namuomba Mola wangu na namuomba msamaha kutokana na yale yaliyonipita. Naomba kufutiwa kwa yale yaliyonipita na ni kipi kinachonilazimu; je, nalazimika kutoa kafara pamoja na kuomba msamaha au nifanye nini?

Jibu: Hakuna kinachomlazimu isipokuwa kutubu, jambo ambalo amekwishalifanya na himdi zote anastahiki Allaah. Halazimiki kurudi kuswali wala kufunga zile swalah na swawm zilizompita. Lakini kuhusu zakaah ni lazima kwake kuzitoa. Asipofanya hivo hakuna neno. Kwa sababu alipoacha swalah alikuwa ni mwenye kuritadi na akawa ni miongoni mwa wanawake wa kikafiri. Hivi sasa Allaah amemuongoza katika Uislamu na ni muislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1389
  • Imechapishwa: 01/12/2019