Mwanamke ameswali ijumaa kama wanaume

Swali: Nilikuwa nikiswali swalah ya ijumaa kama wanavyoswali wanaume Rak´ah mbili na Rak´ah mbili faradhi. Lakini nimesoma kwenye kipeperushi ya kwamba mwanamke hana swalah ya ijumaa. Je, nimekosea?

Jibu: Umekosea juu ya yaliyopita. Kwa sababu swalah ya ijumaa haisihi kwa mwanamke isipokuwa ikiwa kama atahudhuria pamoja na wanaume. Akihudhuria na akaswali pamoja na wanaume basi swalah yame imesihi hali ya kuwa ni yenye kufuata.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (01/354)
  • Imechapishwa: 11/01/2020