Mwanamke amesahau kupunguza nywele baada ya ´Umrah

Swali: Mwanamke alifanya ´Umrah pamoja na mume wake na alisahau kupunguza nywele zake na baadaye akarudi katika mji wake. Kipindi hicho walifanya jimaa. Ni ipi hukumu juu ya hilo?

Jibu: Hukumu ni kwamba anatakiwa kupunguza nywele zake popote alipo. Wakati atapokumbuka au atapojua, basi atapunguza nywele zake, ni mamoja yuko ar-Riyaadh au pahali pengine. Upunguzaji na unyoaji hakuna sehemu maalum, mawili hayo yanafaa kila mahali.

Kuhusu jimaa yake, atalazimika kutoa fidia kwa sababu amefanya makatazo miongoni mwa makatazo ya Ihraam. Fidia hiyo atachinja kondoo Makkah, au atamteua mtu wa kumchinjia, baadaye aigawe kwa mafukara.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 30/05/2020