Mwanamke amelazimika kusafiri bila Mahram

Swali: Kuna dada ambaye amelazimika kusafiri pasi na Mahram. Ni ipi hukumu ya safari hii?

Jibu: Kanuni inasema:

“Dharurah inahalalisha vilivyokatazwa.”

Inafungamanishwa kwa kanuni nyingine isemayo:

“Dharurah inakadiriwa kwa kiwango chake.”

Kanuni hii imechukuliwa kutoka katika Aayah inayosema:

وَقَدْ فَصَّلَ لَكُم مَّا حَرَّمَ عَلَيْكُمْ إِلَّا مَا اضْطُرِرْتُمْ إِلَيْهِ

“… na ilhali ameshakubainishieni yale Aliyokuharamishieni isipokuwa vile mlivyofikwa na dharura navyo.” (06:119)

“Mtu mwenyewe ndiye hukadiria dharurah.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 292
  • Imechapishwa: 04/07/2022