Mwanamke amehiji na kitu kinacholinda mdomo


Swali: Hajj ya mwaka huu nilivaa kitu kinacholinda mdomo. Nilimuuliza kiongozi wa msafara juu ya hilo ambapo akasema kuwa hakuna neno. Niliporudi nikaambiwa kuwa haijuzu kuivaa. Je, kuna kinachonilazimu hivi sasa?

Jibu: Hakuna kinachokulazimu. Ulivaa kitu kinachoulinda mdomo kutokamana na vumbi na vyenginevyo. Hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (84) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17577
  • Imechapishwa: 28/12/2017