Mwanamke amefanya jimaa mara nyingi mchana wa Ramadhaan eti kwa kutokujua

Swali: Mimi ni mwanamke ambaye nilikuwa nimeolewa na mwanaume ambaye alinijamii mchana wa Ramadhaan mara nyingi. Sikuwa ni mwenye kujua jambo hili. Nikahuzunika na nikenda kwa familia yangu kisha nikarejea kwake. Baada ya hapo akanitaliki. Mambo haya yamepitika miaka mingi nyuma pengine ni zaidi ya miaka kumi. Nilikaa naye mwaka mmoja. Je, kuna jambo linalonilazimu juu ya hilo?

Jibu: Ikiwa mwanamke huyu hajui kuwa jimaa ni haramu – kama ilivyo haramu kula na kunywa – basi hakuna kinachomlazimu. Hakuna juu yake kulipa wala kutoa kafara. Lakini ninavofikiria ni kwamba jambo hili liko mbali. Ni jambo liko mbali mwanamke au mwanaume kutokujua ya kwamba ni haramu kwa aliyefunga kufanya jimaa. Ama ikiwa alikuwa anajua kuwa ni haramu lakini hata hivyo hajui ni kipi kinachomlazimu endapo atafanya hivo, basi ni mwenye kupata dhambi na anatakiwa kutoa kafara ambayo ima ni kuacha mtumwa huru, asipopata basi afunge miezi miwili mfululizo, asipoweza basi awalishe masikini sitini. Wanachuoni wamesema kwamba ikiwa alifanya jambo hilo mara nyingi basi ni lazima kwake kutoa kafara kwa kila siku moja aliyofanya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (63) http://binothaimeen.net/content/1451
  • Imechapishwa: 02/01/2020