Mwanamke amechelewesha Shawwaal kwa sababu ya udhuru wa Kishari´ah

Swali: Mwanamke akiwa na deni la Ramadhaan inafaa kwake akatanguliza siku sita za Shawwaal kabla ya deni au deni la Ramadhaan kabla ya siku sita za Shawwaal?

Jibu: Mwanamke asifunge siku sita za Shawwaal akiwa yuko na deni la Ramadhaan kabla ya kumaliza kulipa deni lake. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayefunga Ramadhaan kisha akaifuatishia siku sita za Shawwaal basi ni kama ambaye amefunga mwaka mzima.”

Yule mwenye deni la Ramadhaan hazingatiwi kuwa ameifunga Ramadhaan. Hivyo hapati thawabu za kufunga siku sita za Shawwaal isipokuwa baada ya kumaliza kulipa deni lake.

Lau tutakadiria kuwa ulipaji umechukua Shawwaal nzima, kwa mfano mwanamke hakufunga siku hata moja ya Ramadhaan kwa sababu alikuwa na damu ya uzazi Ramadhaan nzima, kisha akaanza kufunga siku sita za Shawwaal na asimalize isipokuwa baada ya kuingia Dhul-Qa´dah, ana ruhusa ya kufanya hivo. Analipwa thawabu za siku sita za Shawwaal kwa sababu alichelewesha kwa sababu ya dharurah na udhuru. Hivyo atalipwa ujira.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/19)
  • Imechapishwa: 07/06/2019