Mwanamke aliyetwahirika anachelea kumalizika kwa muda wa swalah

192- Nilimuuliza baba yangu juu ya mwanamke ambaye amesafika na ada yake ya mwezi punde tu kabla ya muda wa swalah kumalizika wakati wake; akioga muda utamalizika. Afanye nini?” Akajibu:

“Anayo maji. Anatakiwa kuoga.”

193- Nikamwambia baba yangu:

“Afanye nini akiwa safarini na anachelea muda wa swalah kumalizika akianza kutafuta maji?”

Akajibu:

“Afanye Tayammum na kuswali.”

194- Nikauliza:

“Vipi ikiwa anaweza kununua maji?”

Akajibu:

“Ima anunue maji au afanye Tayammum na kuswali.”

Amesema tena:

“Ayanunue kulingana na fedha zake.”

Nikauliza:

“Ikiwa hawezi kununua maji?”

Akajibu:

“Allaah anasemehe.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin Ahmad bin Hanbal
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad (1/145-146)
  • Imechapishwa: 26/03/2021