Mwanamke aliyefiliwa kabla ya kuingiliwa na mumewe

Swali: Mke akifiliwa na mume wake kabla ya kumwingilia atamrithi mwanaume huyo, atakaa eda na ana haki ya mahari?

Jibu: Ndio. Akimuoa kisha akafa kabla ya kumwingilia atamrithi. Atatakiwa kukaa eda. Ana haki ya kupata mirathi. Ana haki ya mahari yake aliyotajiwa. Ikiwa hakumtajia mahari basi ana haki ya kupewa mahari mfano wa wanawake kama yeye[1]. Kama ilivyothibiti katika Hadiyth kutoka kwa Ma´qiyl bin Sinaan al-Ashja´iy na pia ndivo alivyofutu Ibn Mas´uud. Anapofariki mume kabla ya kumwingilia na kabla ya kumtajia mahari basi atapewa mahari mfano wa wanawake kama yeye. Hatopunguziwa na wala hatopunguziwa. Atakaa eda na atapata mirathi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/66-faida-mbili-kuhusu-masuala-ya-eda/

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ad-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/3557/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%8A%D8%AA%D9%88%D9%81%D9%8A-%D8%B9%D9%86%D9%87%D8%A7-%D8%B2%D9%88%D8%AC%D9%87%D8%A7-%D9%82%D8%A8%D9%84-%D8%A7%D9%84%D8%AF%D8%AE%D9%88%D9%84-%D8%A8%D9%87%D8%A7
  • Imechapishwa: 16/02/2020