Mwanamke alikuwa hajui kuwa anawajibika kutoa Zakaah ya dhahabu zake na sasa amejua

Swali: Kuna mwanamke anamiliki dhahabu ambazo zimefikisha Niswaab. Na tokea amiliki dhahabu hizi zimeshafanya Hawl sita na hakutoa Zakaah kwa kuwa alikuwa hajui kuwa anawajibika Zakaah[1]. Baada ya kujua alitoa Zakaah ya miaka miwili na kumebaki miaka miwili mingine. Ipi hukumu ya hilo na anawajibika nini?

Jibu: Miaka iliobaki iko juu ya dhimmah yake. Kwa kuwa ni haki ya mafukara. Ataitoa pale ambapo Allaah Atamsahilishia. Katika dhimmah yake kumebaki deni juu yake. Na pale ambapo Allaah Atamsahilishia ataitoa kuwapa mafukara.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/mwanamke-alikuwa-hajui-kuwa-anajibika-kutoa-zakaah-ya-dhahabu-zake-na-sasa-amejua/ 

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=1646
  • Imechapishwa: 24/02/2018