Mwanamke alikuwa akifunga kwa ujinga akiwa na hedhi


Swali: Kuna msichana mdogo ambaye alikuwa akifunga wakati wa hedhi yake kwa ujinga. Ni lipi la wajibu kwake?

Jibu: Ni wajibu kwake kulipa swawm ambayo alikuwa akifunga wakati wa hedhi yake. Kwa kuwa funga wakati wa masiku ya hedhi yake haikubaliwi na wala hasihi hata kama alikuwa ni mjinga. Kulipa hakuna mpaka wa wakati wake.

Hapa kuna swali ambalo ni kinyume na hili: Mwanamke amejiwa na hedhi akiwa mdogo. Akaona haya kuambia familia yake. Matokeo yake akawa hafungi. Huyu ni wajibu kwake kulipa mwezi ambao hakufunga. Kwa kuwa mwanamke anapopata hedhi basi ´ibaadah zinakuwa ni zenye kumuwajibikia. Kupata hedhi ni moja katika alama za kubaleghe.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/92)
  • Imechapishwa: 02/06/2017