Swali: Ambaye amepewa mtihani wa kuvuta sigara lakini hata hivyo hadhihirishi hayo mbele ya watu ni mongoni mwa mawalii wa Allaah? Mtu kama huyu aendelee kutafuta elimu?

Jibu: Kama tulivyotangulia kusema kuna watu wamekusanya baina ya mapenzi na uadui. Katika hali hiyo anakuwa na mapenzi kwa Allaah kwa kiasi cha imani na ´Aqiydah sahihi alionayo na vilevile anakuwa na uadui kwa kiasi cha uhalifu alionao.

Sigara ni maasi. Akiendelea kuvuta sigara inapunguza mapenzi yake kwa Allaah (´Azza wa Jall). Lakini hata hivyo hatusemi kuwa ni adui wa Allaah. Tunasema ana mapenzi pungufu kwa kiwango cha dhambi alionayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 07/10/2016