Mwanafunzi muhitaji ana haki zaidi ya swadaqah na zakaah

Swali: Inafaa kwa mwanafunzi ambaye anachelea machafu juu ya nafsi yake kula katika pesa ya zakaah na swadaqah ili zimsaidie kujioza mwenyewe?

Jibu: Ambaye anahitajia kuoa anapewa katika pesa ya zakaah hata kama ni mwanafunzi. Akiwa mwanafunzi yeye ana haki zaidi. Kwa sababu kuoa ni miongoni mwa mambo ya kidharura. Kama ambavo mtu anapewa zakaah kwa ajili ya matumizi, mavazi na makazi basi vivyo hivyo anapewa mtu mahari ambayo ataoa kwayo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 18/09/2020