Mwanafunzi hajitoshelezi na kitabu “Qaa´idah Jaliylah”

Swali: Kijitabu hiki kinamfaa mwanafunzi aliyeanza? Ni ipi tofauti kati ya kitabu hichi na vitabu vyengine vya ´Aqiydah?

Jibu: Katika kitabu hiki kuna ufafanuzi usiopatikana katika vitabu vyengine. Kuna ufafanuzi na kuraddi utata, jambo ambalo pengine linaweza lisipatikane katika vitabu vyengine kwa sura na njia kama hii. Mwanafunzi kukisoma ni katika mambo ya kidharurah makubwa. Kwa kuwa leo – kama mnavojua – waabudia makaburi wana utata mwingi. Hivyo mwanafunzi anahitajia kitu atachojikinga na utata huu na kuuraddi. Angalau kwa uchache asidanganyike na utata huu pale atakapousikia. Awe na kitu cha kuzivunja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2104
  • Imechapishwa: 28/06/2020