Mwanafunzi anatakiwa kupangilia muda wake


Swali: Tumesikia kwamba yule anayetaka kuchuma elimu yenye manufaa basi ni lazima kwake kutenga wakati wa faradhi. Ni upi usahihi wa ibara hii? Ikisihi ni ipi njia ya kulifikia hilo?

Jibu: Kwa hali yoyote mtu anatakiwa ajipangie wakati wake kwa kiasi na anavyoweza. Kwa mfano kwanza anatakiwa apange vitabu anavyotaka kusoma. Kabla ya kila kitu anatakiwa kukifahamu Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall). Kwa sababu  Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ

“Kitabu Tumekiteremsha kwako, hali ya kuwa ni chenye baraka, ili wapate kuzingatia kwa makini Aayah zake.” (38:29)

Hili ni kabla ya kila kitu. Lakini hakuna neno akaongeza juu ya hilo baadhi ya Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha maneno ya wanachuoni katika Tawhiyd na sifa za Allaah na halafu maneno ya wanachuoni katika Fiqh. Vilevile hakuna neno akaambatanisha na taaluma hizi kitu katika lugha ya kiarabu. Lugha ya kiarabu hii leo inakaribia kuwa ni kitu kilichosuswa kwa wanafunzi wengi. Utampata mwanafunzi ambaye tayari yuko mbele katika elimu lakini hata hivyo akisoma utaona makosa mengi katika kisomo chake. Vivyo hivyo pale anapoandika utapata makosa mengi katika maandishi yake. Haya hayatakikani. Kwa hali yoyote mwanafunzi anatakiwa asome chini ya mwanachuoni ambaye atamwelekeza katika yale anayotakiwa kuanza nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (38) al-Liqaa' ash-Shahriy (38) http://binothaimeen.net/content/860
  • Imechapishwa: 27/06/2018