Nawausia wanafunzi wote wawe ni viigizo vyema katika tabia zao, matendo yao na wanaponlingania katika dini ya Allaah ili matendo haya yachangie watu kuikubali Shari´ah ya Allaah. Asiyekuwa msomi anaweza kuikataa Shari´ah ya Allaah kutokana na mwenendo mbaya wa yule anayelingania katika dini ya Allaah. Kwa ajili hii utaona kuna mtu asiyekuwa msomi, lakini wakati huohuo akawa na tabia njema, amezivutia nyoyo za watu. Upande mwingine utaona mtu ni msomi na amebobea katika elimu, lakini hata hivyo hana tabia njema, akawa hapendwi na watu kwa sababu ya tabia yake mbaya.

Kwa hiyo mwanafunzi anatakiwa kutangamana na watu kwa tabia njema ili awe ni mwenye kukubaliwa na Shari´ah ikubaliwe kutoka kwake ambayo Allaah amekutunuku kwa kukujuza nayo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (26)
  • Imechapishwa: 22/01/2019