Mwanafunzi anataka kuomba msaada wa kuoa


Swali: Mimi ni kijana ambaye nina haja kubwa ya kuoa. Hakuna ninachomiliki isipokuwa tu  pesa ya ada ya shule. Inajuzu kwangu kuwaomba watu wa kheri wanisaidie?

Jibu: Ndio, hakuna neno. Ni sawa ukaomba. Lakini endapo utajizuia na ukatendea kazi yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Enyi kongamano la vijana! Yule atakayeweza miongoni mwenu kuoa basi na aoe. Yule asiyeweza basi ni juu yake afunge. Kwani kwake ni kinga.”[1]

ni sawa. Huyu inaonyesha ana haja kubwa. Ikiwa mtenda wema huyu kweli anawasaidia vijana basi anapata thawabu. Hakuna neno akambainishia ya kwamba yeye ni muhitaji. Kuoa ni miongoni mwa mambo yenye umuhimu sana. Ni katika mambo ya udharurah mkubwa. Ni kama mfano wa haja ya kula na kunywa au zaidi ya hivo.

[1] al-Bukhaariy (1905), Muslim (1400), at-Tirmidhiy (1081) na wengineo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alharamain.gov.sa//index.cfm?do=cms.AudioDetails&audioid=63284&audiotype=lectures&browseby=speaker
  • Imechapishwa: 16/09/2017