Mwanafunzi anasema kuwa adhaana ya ´Uthmaan ni Bid´ah

Swali: Tuna mwanafunzi muhindi ambaye anasema kuwa adhaana ya kwanza siku ya ijumaa ni Bid´ah kama Bid´ah ya mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, inajuzu kusoma kwa mtu huyu?

Jibu: Hapana. Sio Bid´ah. Adhaana ya kwanza ilianzishwa na ´Uthmaan ambaye ni khaliyfah wa tatu mwongofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Jilazimieni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu baada yangu. Ziumeni kwa magego yenu.”[1]

Mwanamume huyu ni mjinga. Hatambui Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala haki ya makhaliyfah waongofu.

[1] Abu Daawuud (4607), at-Tirmidhiy (2676) na Ibn Maajah (34). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Irwaa’” (2455).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (71) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah26-07-1438h%20-%20Copy.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2017