Mwanafunzi anakusanya swalah kwa uzito wa kuamka ´Aswr

Swali: Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu ambaye nakusanya swalah wakati wa mitihani na baada ya kumaliza mitihani kwa kuswali chumbani kwake Dhuhr na ´Aswr kwa kukusanya kwa sababu ya uzito wa kuamka katika swalah ya ´Aswr. Unasemaje juu ya kukusanya huku?

Jibu: Naona kuwa kukusanya huku ni haramu. Lau angelikuwa na kazi tusingelimkataza. Ni vipi atalala na kutoswali swalah ya Dhuhr? Kwa hivyo ni wajibu kwake kuswali Dhuhr kwa wakati wake na kuswali ´Aswr kwa wakati wake. Iwapo tungelifanya wepesi kwa watu na kuwaambia kwamba yule aliye na usingizi basi alale na akusanye swalah basi kungelitokea shari kubwa kwa watu. Tunamwambia mwanafunzi huyu aswali Dhurh kwa wakati wake na ´Aswr kwa wakati wake na aache uvivu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (32) http://binothaimeen.net/content/716
  • Imechapishwa: 23/11/2017