Mwanafunzi amekata tamaa kuijua sarufi (النحو)


Swali: Mimi ni mwanafunzi ninayeanza ambaye ambaye najaribu kuielewa sarafi. Lakini hata hivyo nimefikia kiwango cha kukata tamaa. Naomba unielekeze njia bora kuweza kuielewa kwa wepesi? Ni kipi kitabu bora kwa ambaye anaanza? Je, ni lazima kukisoma kwa mwalimu?

Jibu: Inasemekana kwamba kuna mwanachuoni mmoja katika wanachuoni wa sarufi ambaye yalimfika haya yaliyomfika mtu huyu. Alishindwa kuelewa sarufi. Siku miongoni mwa siku akaona mdudumchungu ambaye alikuwa amebeba chakula na anataka kupanda nacho ukuta. Kila anapopanda nacho ukuta anaanguka yeye na chakula chake kwa sababu ya kushindwa. Akafanya hivo mara nyingi. Anajaribu kupanda anaanguka, anajaribu kupanda anaanguka, anajaribu kupanda anaanguka. Mwishowe akapanda na akaweza. Mwanachuoni yule akasema mdudumchungu huyu amejibidisha kazi hii kwa kiwango hichi na hatimae hakukata tamaa na akafikia lengo lake. Ni kwa nini mimi nisimuige? Akamuiga kwa kusoma sarufi na mwishoni akawa ni kiongozi wa sarufi.

Namwambia ndugu yetu muulizaji kwamba miongoni mwa vitabu vizuri, bora na vyenye manufaa zaidi nilivyosoma ni kitabu “al-Ajrumiyyah”. Kitabu hiki ni kifupi na chenye baraka. Mwandishi (Rahimahu Allaah) amekusanya  ndani yake misingi ya sarufi. Midhali wewe ndio unaanza basi lazimiana na kitabu hiki. Fanya bidii upate mwalimu mzuri ambaye anaweka wazi zile maana katika kuyaswawirisha masuala. Inasemwa kuwa sarufi mlango wake ni kama chuma na yaliyobaki ni kasiri bi maana mepesi. Wewe mtake msaada Allaah na jifunze na usikate tamaa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa' ash-Shahriy (37) http://binothaimeen.net/content/846
  • Imechapishwa: 18/04/2018