Sufyaan bin ´Abdillaah ath-Thaqafiy amesimulia:

“Nilisema: “Ee Mtume wa Allaah! Nambie kuhusu Uislamu neno ambalo sintomuuliza baada yako mwengine.” Akasema: “Sema: “Nimemwamini Allaah kisha nyooka barabara.”

Ameipokea Muslim.

Mtu yule alimuomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno yaliyokusanya wema wote, yenye kunufaisha na yatayomfikisha mwenye nayo katika mafanikio. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha amwamini Allaah ambako kumekusanya kila kile ambacho ni wajibu kukiamini kama vile kumwamini Allaah, misingi yake na yaliyo chini ya hayo katika matendo ya kimoyo, kunyenyekea, kujisalimisha kwa ndani na kwa nje. Kisha mtu adumu juu ya hilo na mtu awe na msimamo mpaka wakati wa kufa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bahjatu Quluub-il-Abraar, uk. 13
  • Imechapishwa: 25/01/2019