Swali: Dada huyu  anafunza katika masomo ya wasichana na yuko pamoja na maustadhi wanaume. Dada huyu anapata dhiki kwa uwepo wao. Je, aache kusomesha au aendelee?

Jibu: Naona kuwa katika hali hii aache kusomesha kutokana na dhiki hii anayohisi. Isipokuwa ikiwa wanawake ambao anawasomesha katika masomo haya wana sehemu yao maalum na hawachanganyikani na wanaume. Katika hali hii hakuna neno. Hakuna neno yeye na mume wake wakasomesha katika masomo moja ikiwa wanaume na wanawake kila wamoja wana sehemu zao maalum na hakuna jinsia moja inayochanganyikana na nyingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (05) http://binothaimeen.net/content/6683
  • Imechapishwa: 30/10/2020